Thursday, 4 January 2018

Bunge la Misri limepiga kura kupitisha muswada juu ya Jerusalem

Bunge la Misri limepiga kura juu ya sheria ya Jerusalem, hatua ambayo imekiuka maazimio ya kimataifa yanayohusu mji huo wenye migongano.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Misri Bw. Ahmed Abu Zaid amesema upigaji kura huo, umekiuka sheria za kimataifa kuhusu hadhi ya Jerusalem ukiwa mji unaokaliwa. Ameongeza kuwa mswada huo umekuwa kizuizi kwa mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel, na kuleta ufumbuzi wa haki wa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.
Hatua hiyo ya Israel inakuja baada ya chama cha Likurd kupitisha kwa kura nyingi rasimu ya pendekezo linalowataka wabunge wa Israel wakubali kutwaa makazi ya waisrael katika ukanda wa maghiribi na Jerusalem inayokaliwa.

0 comments:

Post a Comment