Saturday 7 April 2018

Meek Mill kupata dhamana



'Waswahili husema samaki mkunje angali mbichi' swala hili linaenda sawia na msanii kutoka nchini Marekani Meek Mill baada ya kunyimwa dhamana kutoka jela kutokana na Hakimu anayesimamia kesi yake huenda mambo bado yakaenda sawa kwa upande wa rapper huyo wa ‘Win and Losses’
 

Mwanasheria mkuu wa mji wa Philadephia, Lawrence Kranser ametoa ruhusa ya dhamana ya Meek Mill hivyo kwasasa dhamana hiyo itaamuliwa na Mahakama kuu.

Hakimu anayesimamia kesi hiyo Genece Brinkley ndo alikuwa kikwazo kikubwa, April 3 Brinkley alikataa kumpa Meek Mill dhamana na alisema anastahili kabisa kwenda jela kwa miaka 2-4. Hatahivyo kwasasa hana mamlaka hayo tena kwasababu kesi imeamishiwa Mahakama Kuu

Timu ya wanasheria wa Meek Mill inaendelea kupambana huku ikipewa backup kubwa na ushahidi walionao, Polisi aliyemkamata Meek Mill, Reginald Graham alitajwa kwenye orodha ya polisi wala rushwa na wachafu ambayo inajulikana hadi kwa mwanasheria mkuu wa Philadephia.

Timu ya Meek Mill pia imewahi kumtuhumu hakimu wa kesi hiyo, Brinkley kuwa na matatizo binafsi na Meek Mill kwasababu alikataa kumpa rushwa aliyokuwa akiitaka. Pia wametaka hakimu huyo aondolewe kwenye kesi hiyo.

0 comments:

Post a Comment