Tuesday 2 January 2018

China yapiga marufuku uuzwaji bidhaa zitokanazo na pembe za wanyama


China imeidhinisha rasmi sheria ya kupiga marufuku uuzwaji na uchakataji wa aina yoyote wa bidhaa zitokanazo na pembe za wanyama nchini humo.

Balozi wa Kampeni ya kimataifa ya kuzuia ujangili husuani wa Tembo duniani (WILDAD), Yao Ming, ambaye ni Mchezaji wa zamani wa ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani NBA, ikiwajumuisha pia David Beckham, Leonardo Dicaprio, Prince William, Ali Kiba, JackieChan, na wengineo, amesema hatua hiyo ni kubwa kwa serikali ya China.

China ambayo ni moja ya soko kubwa la Pembe za Ndovu kutoka Afrika na duniani, mnamo mwaka 2016 ilitangaza kuwa ifikapo mwisho wa mwaka 2017 itapitisha sheria kukomesha biashara hiyo nchini mwake.

Sheria hiyo inakomesha pia biashara ya mtandao na kwa atakayekutwa na hatia anakabiliwa na kifungo cha miaka kumi mpaka maisha jela.

Uhitaji wa pembe hizo katika soko la ndani la China, umeripotiwa kuchochea ujangili dhidi ya Tembo hususani katika nchi za Tanzania na Kenya.

0 comments:

Post a Comment