Rekodi mpya ya ubingwa mara nyingi
kwenye michuano ya tennis ya Australia iliyokuwa iliyotabiriwa
kuandikwa mwaka huu na Novak Djokovic wa Serbia, imetoweka baada ya
mchezaji huyo kufungwa jana katika mechi ya raundi ya nne ya michuano
hiyo.
Djokovic alifungwa na Chung Hyeon wa Korea Kusini kwa seti ya 3-0
yenye alama 7-6 7-5 na 7-6, na kumfanya asalie na rekodi yake ile ile ya
kushinda taji hilo mara sita ambayo ni sawa na iliyowekwa na Mzee Roy
Emerson aliposhinda mfululizo kuanzia mwaka 1960-1965.
Katika mechi zingine zilizopigwa jana, bingwa mtetezi, Roger Federer wa Uswisi alimshinda Márton Fucsovics wa Hungary kwa seti ya 3-0, na kufuzu hatua ya robo fainali ambako huko atakutana na Tomas Berdych kutoka Jamhuri ya Czech.
Endapo Federer atashinda taji hili kwa mwaka huu, ataifikia rekodi ya Djokovic na Emerson kwani mpaka sasa ameshinda mara 5.
Na michuano hiyo inaendelea leo, ambao kipekee mchezaji namba moja kwa viwango vya ubora kwa sasa, Rafael Nadal wa Hispania anacheza mechi ya robo fainali na Marin Cilic wa Croatia ambaye ni namba 6 kwa ubora duniani kwa sasa.

0 comments:
Post a Comment