Tuesday 6 February 2018

ANC kumweka kikaangoni Zuma


Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeitisha mkutano wa viongozi wake wa juu siku ya jumatano,huku kukiwa na taarifa kwamba mkutano huo ni kwaajili ya kujadili shinikizo lakumtaka rais Jacob Zuma kuachia madaraka.
Hata hivyo kauli ya cha cha ANC iliyotolewa kuhusiana na mkutano huo imesema kuwa,wanakutana kujadili ubadilishanaji madaraka kutoka Rais Zuma kama mwenyekiti wa zamani na sasa Cyril Ramaphosa ambaye ni kiongozi mpya wa chama hicho.
Siku ya jumatatu viongozi wandamizi wa chama hicho walilazimika kuwa na mkutano wa dharula mjini Johannesburg kujadili hatima ya rais Zuma.
Hata hivyo rais Zuma ameshikilia msimamo wake kutokubaliana na shinikizo la kumtaka aachie madaraka.
Mwezi Disemba mwakajana Ramaphosa alimrithi rais Zuma katika nafasi ya juu ya kukiongoza chama hicho kikongwe barani Afrika.
Nafasi ya urais ya Zuma imekuwa ikiandamwa na kashfa za rushwa,ambapo katika miaka ya hivi karibuni alihusishwa na familia yenye asili ya India ijulikanayo kama Gupta ambapo inadaiwa alitumia madaraka yake vibaya ili kujinufaisha yeye na washirika wake hao.

0 comments:

Post a Comment