Sunday 11 March 2018

China wapitisha zuio la kuongza ukomo wa urais



Bunge la nchini China limepiga kura kupitisha marekebisho ya Katiba na kuondoa ukomo wa rais kukaa madarakani. Rais wa sasa Xi Jinping aruhusiwa kutawala bila kikomo

Katika mchakato huo uliohusisha Wabunge takribani 3000 waliopiga kura na wakati wa kutolewa kwa matokeo ni Wabunge wawili tu ndio walipiga kura ya hapana dhidi ya mabadiliko hayo
Katiba ya China ilikuwa ikitoa uhalali kwa Rais kukaa madarakani kwa muda usiozidi vipindi viwili tu huku kila muhula ukiwa hauzidi miaka 5(kama ilivyo kwa Katiba ya Tanzania)
Mwezi uliopita chama cha Kikomunisti cha China kinachoongoza taifa hilo kilitoa pendekezo la kuondolewa kwa ukomo wa mihula ya Rais na Makamu wa Rais na leo wamehitimisha kwa kupiga kura

0 comments:

Post a Comment