Mwanadada Venus Williams
amefanikiwa kumfunga mdogo wake Serena Williams hatua ya raundi ya tatu
ya michuano ya Indian Wells na kuwa mwisho wa safari ya Serena katika
michuano hiyo tangu arejee katika tenisi baada ya uzazi.
Serena aliyewahi kuwa mchezaji namba moja kwa ubora duniani amepoteza
mchezo huo kwa jumla ya seti 6-3, 6-4. Venus yeye amefanikiwa kusonga
mbele hadi raundi ya 16 ambapo atakabiliana na Anastasija Sevastova.
0 comments:
Post a Comment