Klabu za Soka za Sevilla ya Uhispania na AS Roma ya Italia jana usiku zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali katika michuano ya Klabu Bigwa barani humo
Sevilla wamefuzu baada ya kuitandika Manchester Utd goli 2-1 katika mechi ya marudiano kwenye uwanja wa Old Traford baada kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uhispania
AS Roma jana akiwa katika uwanja wa nyumbani alipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk katika mechi ya marudiano . Mechi ya kwanza Shakhtar alipata ushindi wa goli 2-1. Roma anafuzu kwa sheria ya goli la ugenini
Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo Barcelona anakutana na Chelsea katika uwanja wa Camp Nou, huku Besiktas anakutana na Bayern Munich
0 comments:
Post a Comment