Monday 12 March 2018

Sudan na Qatar zaweka mstakabali suala la Darfur


Sudan na Qatar zimefanya majadiliano kuhusu suala la amani kwenye eneo la Darfur, na kufuatilia mchakato wa amani wa Darfur.
Rais Omar al-Bashir wa Sudan alikutana na naibu waziri mkuu wa Qatar Bw. Mohamed al-Thani huko Khartoum. Bw. Al-Thani amewaambia waandishi wa habari kuwa walijadili kuhusu suala la amani la Darfur na kufuatilia mchakato wa amani wa Darfur. Wote walifurahishwa na makundi mengi kutaka kujiunga na makubaliano ya Doha.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ibrahim Ghandour amesema makubaliano ya Doha ni njia pekee ya amani Darfur, nchi hizo mbili zilijadili kuhusu kuhitimisha makubaliano ya Doha, hasa ukarabati huko Darfur.

0 comments:

Post a Comment