Thursday 12 April 2018

Marekani yaitahadharisha Urusi juu ya Syria

  Rais Donald Trump ameiambia nchi ya Urusi kwamba ijiandae maana Marekani itashambulia nchi ya Syria kwa makombora mapyaMarekani imeazimia kuishambulia Syria baada ya kuituhumu serikali ya nchi hiyo kushambulia kwa kemikali za sumu eneo la waasi la Douma na kusababisha vifo vya watu kadhaa siku 4 zilizopita

Urusi ambayo ni rafiki wa Rais wa Syria Bashir al-Assad iliionya Marekani kwamba itazuia makombora yoyote ya Marekani yatakayoshambulia Syria na kwamba watashambulia sehemu makombora hayo yatakapotokea

Aidha, Rais Trump amesema uhusiano baina ya nchi yake na Urusi ni mbaya kuliko ulivyowahi kuwa na kwamba kwa sasa inahusisha vita baridi

0 comments:

Post a Comment