Thursday 12 April 2018

Ndege yaanguka nchini,Yaua 250 Algeria



Nchini Algeria Takribani watu 250 wamefariki dunia baada ya ndege ya Jeshi kuanguka karibu na uwanja wa ndege wa Boufarik, nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo Algiers

Taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea Mji wa Bechar uliopo magharibi mwa Aligeria ilikuwa imebeba vikosi vya wanajeshi vya takribani watu 20 kila kimoja

Hii ni ajali mbaya ya ndege kuwahi kutokea nchini Algeria tangu mwaka 2003 ambapo ndege ilianguka katika uwanja wa Tamanrasset muda mfupi baada ya kuruka na kuua watu 102

0 comments:

Post a Comment