Tuesday 24 April 2018

SportPesa yarudi kufandhili soka nchini Kenya


Kampuni ya kubashiri mchezo SportPesa, imerejesha ufadhili wa ligi kuu ya soka nchini Kenya KPL. Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa Ronald Karauri amesema kampuni yake itatoa Shilingi Milioni 685 kufadhili soka nchini humo kwa muda wa miaka mitatu ijayo.
Kati ya fedha hizo, Shirikisho la soka FKF, itapata Shilingi Milioni 69 huku ligi kuu KPL ikipangiwa Milioni 259.
Mwaka uliopita, SportPesa ilijiondoa katika ufadhili wa michezo nchini humo baada ya serikali kuitaka kulipa kodi ya asilimia 35 kutoka kwa mapato inayokusanya kila mwaka. Hata hivyo, SportPesa haitaendelea na ufadhili wa michezo ya raga na bondia kama ambavyo ilikuwa inafanya hapo awali.

0 comments:

Post a Comment