Saturday 14 April 2018

Telegram kufungiwa nchini Urusi




Huko Nchini Mahakama yaamuru kufungiwa kwa mtandao wa Telegram baada ya kuridhia madai ya Mamlaka ya Mawasiano(Roskomnadzor)

Roskomnadzor iliyodai kuwa Telegram imeshindwa kutoa ushirikiano kwa kugoma kuiruhusu Serikali kuingilia mawasiliano ya watumiaji nchini humo

Jaji Yulia Smolina amesema kuwa matumizi ya mtandao huo yatafungwa na hakutakuwa na uwezekano wa watu kuwasiliana kwa kutumia mtandao huo(Telegram). Maamuzi haya ya Mahakama lazima yatekelezwa mara moja kuanzia leo hukumu iliposomwa.

Mwanzilishi wa Mtandao huo(Telegram) alinukuliwa mwishoni mwa mwezi uliopita akisema kuwa juhudi za kuwalazimisha kutoa taarifa za siri za watumiaji wake hazitazaa matunda. Telegram itaendelea kulinda usiri wa wateja wake.

0 comments:

Post a Comment