Friday 13 April 2018

Wizkid Kupanda jukwaa moja na Beyonce Kesho,Tuzo Coachella



Jumamosi hii Wizkid atatumbuiza kwenye jukwaa la tamasha kubwa Marekani, Coachella.

Wizkid ambaye amepangiwa kutumbuiza siku ya Jumamosi, atashare stage na Beyonce.

Pia Dj maarufu wa Afrika Kusini, Black Coffee atatumbuiza kwenye tamaisha hilo siku ya Ijumaa siku moja na mastaa wengine marekani kama The Weeknd na SZA.

Pia siku ya jumapili stage hiyo itashambuliwa na wakali wengine ikiwemo Eminem, Cardi B, Miguel, Jidenna, Migos na wengine wengi.

Coachella ni tamasha maarufu la sanaa na muziki Marekani, Umaarufu wake ni mkubwa kwasababu ya mastaa wengi ambao huwa wanaudhulia (hata kama hawaperform) na huwa wanajichanganya na mashabiki, huwa inafanyika weekend nzima.

0 comments:

Post a Comment