Umoja wa Mataifa(UN) umezionya nchi zenye nguvu kutoruhusu mzozo kuhusu madai ya matumizi ya silaha za sumu dhidi ya Syria kuongezeka
Kutokana na hali ya wasiwasi kuhusu mvutano huo wa Syria, mkutano wa faragha wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utafanyika baadae leo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema hadi sasa Baraza la Usalama la umoja huo limeshindwa kufikia makubaliano ya kidiplomasia kuhusu Syria
Urusi na Marekani hadi sasa zimepiga kura ya turufu kupinga azimio la kila mmoja la kutaka kuanzisha uchunguzi wa kimataifa kuhusu matumizi ya silaha za sumu
Shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za sumu, OPCW, limesema hivi karibuni litapeleka timu yake ya wachunguzi kwenye mji wa Douma kwa ajili ya kufanya uchunguzi
0 comments:
Post a Comment