Wednesday 4 April 2018

WTO yaahidi kuunga mkono eneo la biashara huria barani Afrika


Mkurugenzi wa Shirika la Biashara duniani (WTO)Bw. Roberto Azevedo amesema WTO itaunga mkono mipango ya nchi za Afrika kuanzisha eneo la biashara huria.
 
Akiongea na wanahabari mjini Lisbon, Bw Azevedo amesema juhudi za nchi za Afrika kuanzisha eneo la biashara huria hazikinzani na maslahi ya WTO.
Amesema WTO itaunga mkono mchakato wa mafungamano ya nchi za Afrika, na pia kanuni zake zinatakiwa kuunga mkono mafungamano na maendeleo ya bara la Afrika

Eneo la biashara huria la Umoja wa Afrika lilianzishwa mwezi uliopita kwenye mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika nchini Rwanda, kama nchi zote zitaidhinisha kuanzishwa kwa eneo hilo litakuwa eneo kubwa la biashara huria linaloshirikisha nchi nyingi zaidi, mbali na Shirika la biashara duniani.

0 comments:

Post a Comment