Friday 25 May 2018

Childish Gambino ndani ya Black Panther



Mtandao wa Metro Uk umeripoti kuwa director wa filamu ya Black Panther, Ryan Coogler kwasasa yupo kwenye mazungumzo na Donald

Imeripotiwa kuwa coogler ameanza kuandaa cast ya waigizaji ya filamu ijayo, kulikua na tetesi pia kuwa Kendrick Lamar anaweza akatokea kwenye filamu hiyo -
Donald Glover kwasasa yupo vizuri kwasababu mwaka jana ametokea kwenye filamu kubwa ya Spiderman, pia mwaka huu anatokea kwenye filamu ya Star Wars “Solo: A Star Wars Story” ambayo inatoka ijumaa hii, Pia ameingiza mkwanja mrefu kupitia filamu ijayo ya “Lion King” ameigiza kama Simba na Pia Tv show yake ya “Atlanta inafanya vizuri”
-
Kwa upande wa pili wa muziki, Donald Glover ambaye anatumia jina la Chilidish Gambino anashika namba moja na ngoma yake mpya ya “This is America”

0 comments:

Post a Comment