World Most #PowerfulPeople List of @Forbes #forbes
1. Xi Jinping
Jingping amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais Vladimir Putin wa Urusi ambaye kwa sasa anashika nafasi ya pili.
Xi ameonekana kuwa na ushawishi mkubwa sana toka kipindi alipoweza kuwashawishi wabunge takribani 1000 kukubali kupitisha muswada wa kuondolewa kikomo cha kiti cha urais nchini China.
2. Vladimir Putin
Rais wa Urusi, Vladmir Putin kashuka katika nafasi yake ya kwanza lakini haijamuondolea sifa ya kuwa kiongozi mwenye ushawishi, kwa miaka 18 katika utawala wake Putin ahesabiwa kama kiongozi mwenye nguvu zaidi nchini Urusi na ushawishi wa kuwafanya wananchi wake kuwa wazalendo.
3. Donald Trump
Rais wa 45 wa Marekani, licha ya kuwa kiongozi mwenye matamshi ya kuudhi lakini amekuwa mmoja kati ya viongozi aliyeweza kuweka ushawishi mkubwa kwa wafanyabiashara na kusaidia uchumi kuongezeka maradufu nchini Marekani.
4. Angela Merkel
Anatajwa kuwa mwanamke mwenye nguvu zaidi kwenye karne hii, jambo linalomfanya kuwa katika orodha hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuwaunganisha wanasiasa wa vyama vyote hasa wapinzani katika ujenzi wa Taifa la Ujerumani.
5 Jeff Bezos
Tajiri namba moja Duniani na mmiliki wa Kampuni ya Amazon anakuwa tajiri mkubwa mwenye ushawishi kutokana na usadizi wake katika kusaidia vijana wenye vipaji duniani.
6. Pope Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki , kanisa lenye waumizi zaidi ya Bilion Moja Papa Fransic amekuwa mstari wa mbele katika kupinga nchi zinazokiuka haki za binadamu duniani.
7. Bill Gates
Tajiri namba mbili Duniani, kutokana na kuwa mkuu wa kampuni ya Microsoft Bill Gates anakua mmoja kati ya matajiri wanaopigana katika kutokomeza malaria duniani.
8. Mohammed bin Salman Al Saud
Mwanamfalme ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki na kulaan rushwa nchini Saudi Arabia anahesabiwa kama mtu ambaye anaweza kuirudisha heshima katika familia yenye utajiri wa mafuta ya U.A.E
9. Narendra modi
Waziri Mkuu wa India ameshika nafasi ya Tisa mwaka huu,kiongozi huyo wa watu wengi duniani amekuwa katika nafasi ya juu katika ushawishi hasa katika kuimarisha uchumi.
10. Larry Page @Google
10. Larry Page @Google
Ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Google ,kwasasa ni mkurugenzi wa kampuni ya Alphabet ambayo ni tawi la Google.
0 comments:
Post a Comment