Thursday 24 May 2018

Rais wa Ghana kuwashughulikia wabadhirifu katika soka


Rais wa Ghana  Akufo-Addo ameamuru kukamatwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka nchini humo, Kwesi Nyantekyi

Kwesi ambaye pia ni Makamu wa Rais wa kwanza wa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika(CAF)

Rais Akufo-Addo ametoa amri hiyo baada ya Mwenyekiti huyo wa chama cha soka kutuhumiwa kwa ulaghai kwa kutumia jina la rais huyo

Aidha taarifa ya kiuchunguzi iliandaliwa na Mwanahabari maarufu nchini humo, Anas Aremeyaw pia ilifichua vitendo vya ufisadi miongoni mwa maafisa wengine wa shirikisho la soka humo.

0 comments:

Post a Comment