Monday 18 June 2018

Ben Pol kuja na Album



Mkali wa Rnb kwenye bongo fleva, Bernald Paul maarufu kama Ben Pol ametangaza kuandaa album na Kutoa nafasi kwa producers wapya kwenye game katika kuandaa album yake.

"Za leo?, nimeanza kufanyia kazi album yangu mpya, na sasa hivi ningependa pia kutoa nafasi chache kwa producers wapya, kama unahisi una beat kali! Na ungependa kufanya kazi nami kwenye album yangu mpya basi tutumie beat(s) kwa whats app +255738 837755 au kwa email; thisisbenpol@gmail.com, Tutasikiliza kisha tutakaa na wewe mezani. Shukraan 🙏🏽.
Ben Pol" ameandika Ben Pol kupitia Instagram

Ben Pol alitambulika rasmi kwenye game ya bongo fleva mwaka 2010 kupitia nyimbo yake "Nikikupata" na kuchukua tuzo ya msanii chipukizi mwaka 2011 katika Kill Music Awards, na baadae kuachia hit song kama samboira, pata raha, maumivu, pete na zingine kibao mpaka sasa.
.

0 comments:

Post a Comment