Thursday 5 July 2018

BABA AMNYONYESHA MWANAYE BAADA YA MKEWE KUSHINDWA.



Wakati wanandoa huko Wisconsin waliendesha kumkaribisha mtoto wao sio mama tu alikuwa na usiku uliokumbwa na visanga bali baba pia alishiriki kwa njia ambayo hakuwa ameitarajia.

Kujifungua kwake April Neubauer, hakukuwa rahisi kwa sababu alikumbwa na tatizo linalofahamika kama pre-eclampsia, na mpigo wa juu wa damu, hali iliyosababisha akimbizwe chumba cha dharura cha upasuaji.

Wakati mtoto Rosalie alizaliwa tarehe Juni 26, mama yake April alikumbwa na tatizo lingine ndipo akapelekwa kwa matibabu zaidi kabla ya hata kumshika mtoto wake.

Kwa sababu ya hilo mtoto Rosalie ambaye alikuwa na uzani wa kilo 3.6 akakabidhiwa baba yake Maxamilllian. "Muuguzi akaja na msichana wangu mrembo , tukaenda chumba cha watoto, nikaketi na kuvua shati langu ili nimkumbatie mtoto," aliiambia BBC.

Muuguzi akasema kuwa walihitaj kumpa mtoto maziwa ya unga kwanza. "Kisha muuguzi akauliza kama nitaweza kutoa titi langu nimnyonyeshe. Na mimi nikiwa mtu ambaye anapenda kujaribu mambo, nikasema mbona nisifanye hivyo"

Muuguzi akaunganisha mrija ambao ulikuwa umeunganishwa na sirinji iliyokuwa na maziwa ya unga kwa kifua chake Maxamillian.

0 comments:

Post a Comment