Monday 9 July 2018

Justin Bieber amvalisha pete Hailey Baldwin.



According to #Tmz Justin Bieber amemvalisha pete ya uchumba Hailey Baldwin ndani ya mgahawa nchini Bahamas siku ya Jumamosi. Wateja walioshuhudia tukio hilo ndani ya mgahawa wanadai kuwa walinzi wa Justin Bieber waliamuru kila mtu aweke simu yake mbali kwa sababu kuna tukio kubwa Justin anaitaji kufanya mbele yao, na baada ya hapo Justin Bieber alitoa pete ya uchumba na kumvesha Hailey.

Justin na Hailey wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa mwezi mmoja baada ya Justin kuachana na Selena Gomez. Baba Mzazi wa Justin Bieber, Jeremy Bieber kupitia ukurasa wake wa Instagram alimpongeza mwanae kwa tukio hilo alilofanya.

0 comments:

Post a Comment