Monday 9 July 2018

XXXTentancion alisaini mkataba wa dola milioni 10 kabla ya kuuawa



Imeripotiwa kuwa mwanamuziki  XXXTentacion alisaini mkataba wa dola milioni 10 , wiki kadhaa kabla ya kuuawa.

XXXTentancion alitia saini makubaliano ya dola milioni 10 na kampuni ya muziki ya kujitegemea Empire Distribution, iliyotowa albamu yake ya kwanza, kulingana na The New York Times.

Mwanzilishi wa kampuni hiyo ya muziki Ghazi Shami alikataa kuthibitisha mkataba huo wa dola milioni 10 kwa Gazeti la New Yok Times lakini alisikika akisema kuwa "kiasi kikubwa cha fedha" kwa albamu ya tatu ya XXXTentacion tayari imeandikwa. Hata hivyo, muziki mpya huo hauwezi kutoka mpaka Oktoba, kutokana na mkataba uliopita.

0 comments:

Post a Comment