Tuesday 10 July 2018

Mtoto wa Zuma ashtakiwa kwa Rushwa



Mtoto(Duduzane Zuma) wa Rais wa zamani, Jacob Zuma ameshitakiwa kwa makosa ya rushwa katika Mahakama ya biashara mjini Johannesburg.

Duduzane Zuma(34) anadaiwa kuwa sehemu ya waliojaribu kumuhonga Naibu Waziri wa Fedha ili kumshawishi achukue nafasi muhimu za juu kwenye Serikali. Mashitaka hayo pia yanahusishwa na familia maarufu ya Gupta

Hata hivyo Duduzane pamoja na Familia ya Gupta wamekana kuhusika na mashitaka hayo

Mwaka 2015, Naibu Waziri wa Fedha, Mcebisi Jonas alidai kupewa ofa ya nafasi ya Uwaziri wa Fedha na hongo ya 600 milioni rand(takirbani Tsh. Bilioni 100) wakati akiwa kwenye kikao na Duduzane, mfanyabishara Fana Hlongwane na Ajay Gupta

Aidha, Duduzane ambaye anaishi Dubai alirejea nchini humo ili kuhudhuria mazishi ya Kaka yake ndipo akakamatwa na hati yake ya kusafiria kuchukuliwa

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 24, 2019 na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana

0 comments:

Post a Comment