Tuesday 10 July 2018

Waziri wa Mambo ya Nje Uingereza ajiuzuru rasmi



Waziri wa Mambo ya Nje, Boris Johnson ametangaza kujiuzulu wakati nchi hiyo ikiwa kwenye mgogoro uliozuka katika utekelezaji wa mpango wa kujiondoa kutoka katika uanachama wa Jumuiya ya Ulaya 'BREXIT'

Boris anakuwa Waziri wa pili kujiuzulu ndani ya saa chache baada ya Waziri aliyekuwa akishughulikia mpango wa BREXIT, David Davis kujiuzulu

Mawaziri hawa wanajiuzulu wakati ambao Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Theresa May anajiandaa kulihutubia Bunge kuhusu mpango wake mpya juu ya BREXIT

Aidha, ofisi ya Waziri Mkuu imemshukuru bwana Boris na kuongeza kuwa mrithi wake atatangazwa haraka

0 comments:

Post a Comment