Monday 23 July 2018

Tekashi69 alazwa hospital baada ya kutekwa


Mtandao wa #tmz umetoa taarifa ya kutekwa kwa rapper Tekashi69 siku ya leo majira ya saa 10 asubuhi kwa saa za marekani akiwa anafanya shooting ya video yake mpya mitaa ya Brooklyn, New York City.

Wanaume watatu wakiwa na silaha za moto mkononi, walimchukua Tekashi69 na kumuingiza ndani ya gari mpaka nyumbani kwake akiwa seat ya nyuma kwa ulinzi mkali. Tekash69 alipewa masharti ya Kutoa mikufu yake yote ya thamani pamoja na pesa la sivyo wangemuua.

Wanaume wawili walishuka na kuingia ndani ya nyumba ya Tekashi69 na kubeba mikufu yenye thamani ya $750,000 (Tshs billion 1.5) pamoja na hela kiasi chs $20,000 (Tshs Million 41) bila mkudhuru baby mama wa Tekashi69 pamoja na mwanae ambao walikuwa ndani ya nyumba.

Majambazi waliondoka tena na Tekashi69 akiwa amewekwa seat ya nyuma, lakini njiani Tekash69 alifanikiwa kufungua mlango na kujirusha nnje. Mmoja wa majambazi alishuka na kumkimbiza Tekashi69 lakini alimuachia na huenda alihofia kujulikana. .

Tekashi69 alikimbia na kuingia kwenye gari ya mtu kujificha, alisaidiwa na kupiga 911 kupata msaada na kuamliwa ashuke ndani ya gari kwa sababu ya usalama wa mwenye gari. Ambulance ilifika na kumkimbiza hospital na kufanyiwa vipimo mbalimbali kama CT scan.

Blogged by @silverracca

0 comments:

Post a Comment