Monday 8 January 2018

Umezungukwa na watu gani katika kukupa hamasa


Katika maisha yetu ya kila siku tumezungukwa na watu wengi wa aina nyingi, ambao kwa namna moja au nyingine hutupa mchango hasi au chanya.

Kuna aina nne za watu ambazo ni Virusi, Kupe, Uyoga na Asili;

VIRUSI, hawa ni aina ya watu ambao naweza kuwaita pia panya ni watu wenye kuweza kuingia popote na kwa mtu yeyote kwa sura tofautitofauti, ni ngumu sana kuwatambua, watu hawa hujigeuza kuwa marafiki kwa haraka sana, huweza kukufanya uwaamini kwa haraka nia yao kubwa ni kuchukua taarifa ya yale unayoyafanya pamoja na mipango yako nia ni kuivuruga mipango yako au mambo yako unayoyafanya yasifanikiwe kwa kutumiwa na watu wengine au wao wenyewe. Watu hawa pia huweza kuiba mawazo ya wengine kwa urahisi sana na kuyafanyia kazi kama yao. Hapa inatakiwa uwe makini sana watu kama hawa wanatakiwa kuona au kupata matokeo ya shughuli zako na sio mipango yako.

KUPE ni aina ya pili ya watu wanaotuzunguka ambao wao hawana mawazo wala mipango mipya, hawa wanaishi kwa mtindo wa unyonyaji mara nyingi wakiajiriwa kwenye taasisi huzorota au kufa kwani wao huwekeza katika kuchukua tu na sio kuchangia, wao hutengeneza mazingira ya ulaji hawajali watu wengine, kama wapo mahali watahakikisha wanamlinda aliyepo kwenye nafasi anayewahakikishia ulaji kwa garama yoyote, wapo tayari kuwatoa mhanga watu wengine ilimradi wao wanufaike, watu hawa mara nyingi wana uwezo mdogo hivyo hung'ang'ania eneo moja kwa muda mrefu sana

UYOGA, hawa ni kama fisi, wao huangalia udhaifu wa wengine na kuutumia kujinufaisha wao wenyewe. Wapowapo kwamfano husubiria ndugu wanapokufa na kuanza kugombania mali au kuuza mali za urithi, kuuza maeneo ya kijiji, kuuza maeneo au mali za watu walioko mbali

ASILI, hili ni kundi la mwisho, kundi hili ni la watu ambao hupenda kusimama wao kama wao, ni watu wanaojiamini sana, wanaoamini mawazo yao na ni watu wabunifu, aina hii ya watu huwa wapole na wataratibu

NB: Hawa watu wote ni muhimu sana katika maisha na sisi wote lazima tuangukie kwenye kundi mojawapo ili mzunguko wa maisha ukamilike. Cha msingi ni kujitambua kuwa unahitaji nini katika maisha.

0 comments:

Post a Comment