Mlimbwende Ruth Wanjiku ahukumiwa kifo baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kijana aliyekuwa mpenzi wake
Ruth
Wanjiku alimchoma mpenzi wake huyo kisu mara 22. Kabla ya hukumu hii
alikuwa akishikiriwa katika Gereza la Kuu la Wanawake la Lang'ata
Miss
huyo alimuua Farid Mohammed aliyekuwa mpenzi wake mnamo tarehe 20 mwezi
Septemba mwaka 2015 katika eneo la Buruburu Jijini Nairobi
Mlimbwende
huyo alikiri kumuua mpenzi wake huyo kwa kisu kilichokuwa jikoni baada
ya kuzuka kwa mzozo kati yao uliotokana na tuhuma za Mwanaume huyo
kutokuwa mwaminifu
Jaji Jassie Lessit aliyekuwa akiendesha kesi
hiyo wakati akitoa hukumu hiyo alisema hukumu hiyo iwe funzo kwa vijana
na wanapaswa wajue kwamba ‘’si vyema kumuua mpenzi wako, ni vyema
ukaamua kuondoka zako."
0 comments:
Post a Comment