Tuesday, 20 February 2018

ZIWA NGOZI NA MAAJABU YAKE




                         ZIWA NGOZI

Ziwa ngozi ni moja ya vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania katika pande za kusini magharibi mwa Tanzania mkoani Mbeya,wilaya ya Rungwe nchini Tanzania katika kijiji cha Mbeye.

Ziwa hilo linaweza kuwa geni masikioni mwako lakini ni ziwa linalotembelewa na watalii wengi kila mwaka  udhuru ziwa hilo.

Chanzo cha ziwa Ngozi ni mlima na inasemekana kuwa lilipatikana kutokana na mlipuko wa volcano na ndipo lilipoundwa.

Kina kilichopo katika ziwa hilo ni Mita 74 na urefu wa kilomita 2.5 , Muonekano wake ni wa kusisimua kutokana tu na misitu iliyoizunguka huku hali ya hewa ikiwa kiwango cha joto18°C.

Imeandaliwa na Msafiri Ulimali
COOL BONGO ADVENTURE

0 comments:

Post a Comment