Kikoi ni vazi la kiume ambalo mara nyingi huvaliwa nyumbani wakati mtu akiwa amepumzika ,asili ya vazi hilo imetokana na watu wa mwambao wa pwani ambalo wakati mwingine pia hutumika kuvaliwa wakati wenyeji hao wanapokuwa wakicheza ngoma zao za asilin,ikiwamo kibati na kidumbaki.
Katika ngoma ya kibati, wanaume huvaa kikoi huku wakiwa wameshika fimbo aina ya mkongoja huku wanawake wakiwa wamevalia vazi la kanga .
Lakini kutokana na mchanganyiko wa hapa na pale ,vazi hilo limekuwa halina mtu maalum wa kulivaa , kwani hivi sasa kikoi hushonwa na zaidi na jinsia zote katika mitindo mbalimbali .
Hapo zamani kikoi kilionekana ni vazi la wanaume tofauti na ilivyosasa, huku wazee wetu hapo zamani walikuwa wakilitumia vazi hili kuwavalisha wali wakiume siku ya sherehe yao mara baada ya kutoka katika jando.
Lakini pamoj na vazi hili kuvaliwa na jinsia zote, Zanzibar walipiga marufuku uvaaji wa kikoi kwa wanawake kwani waliona ni jambo laa kudhalilisha mavazi ya kiume kwa kusema kwamba haiwezekani kila vazi linalovaliwa na wanaume .
0 comments:
Post a Comment