Iran imeendeleza kupinga mabadiliko yoyote katika mkataba
uliofikiwa kati yake na nchi sita zenye nguvu zaidi duniani baada ya
Rais wa Marekani Donald Trump kutaka hatua zaidi kuhakikisha mkataba huo
unaendelea kutekelezwa.
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema haitakubalia
marekebisho yoyote kufanyiwa mkataba huo sio sasa wala katika siku za
usoni na haitakubali masuala mengine kuhusiswa na mkataba huo wa
kinyuklia uliiofikiwa mwaka 2105 unaojulikana kama mpango wa utekelezaji
wa pamoja JCPOA. Urusi imeionya Marekani kuwa kujiondoa kutoka mktaba
huo itakuwa ni kosa kubwa.Marekani yatilia shaka makubaliano
Makubaliano hayo yanayolenga kuidhibiti Iran kutoendeleza mipango yake ya kuunda silaha za kinyuklia na badala yake iondolewe baadhi ya vikwazo vya kiuchumi yanaungwa mkono na Urusi, Uingereza, Ufaransa, Urusi, Ujerumani na Umoja wa Ulaya isipokuwa tu Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump imekuwa ikitilia shaka utayari wake wa kuendelea kuwa sehemu ya nchi zilizotia saini makubaliano hayo ya JCPOA.
Mnamo siku ya Ijumaa, Trump aliahirisha utekelezaji wa baadhi vikwazo vinavyohusiana na uuzaji wa mafuta na mfumo wa benki wa Iran, akisema amechukuwa tu hatua hiyo ili kupata makubaliano na washirika wa Ulaya ili kurekebisha kasoro zilizomo katika makubaliano hayo.
Trump anataka makubaliano mapya ya kuudhibiti zaidi mpango wa kinyuklia w a Iran utakaojumuisha vikwazo zaidi vinavyolenga vinu vya kinyuklia vya Iran. Hata hivyo nchi nyingine zenye nguvu zaidi duniani zilizoshiriki katika mkataba wa 2015 zinasema makubaliano hayo yanafanya kazi kama ilivyotarajiwa na kuwa Iran inaheshimu na kutimiza yaliyofikiwa katika makubaliano hayo.
Macron asisitiza makubaliano yadumishwe
Siku ya Jumamosi (13.01.2018) Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisisita kuwepo haja ya pande zote zinazohusika kuheshimiana kuhusiana na mkataba huo kati ya Iran na nchi zenye nguvu zaidi duniani akitaka mkataba huo kudumishwa kama ulivyo. Aliyasema hayo katika mazungumzo ya simu aliyoyafanya na Waziri mkuuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
0 comments:
Post a Comment