Mchezaji wa tennis wa Uingereza Andy Murray amejiondoa katika mashindano ya Kimataifa ya Brisbane yanayoendelea nchini Australia kwa kile alichodai kuwa anaendelea kuuguza maumivu ya mgongo aliyopata tangu mwezi Julai mwaka 2017.
Kujitoa kwenye mashindano kunapunguza uthabiti wa maandalizi wa nyota
huyo kuelekea michuano mikubwa ya wazi ya Australia itakayoanza Januari
15 na wasiwasi ukitanda kuwa huenda asishiriki.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashindano ya Brisbane Bw. Cameron Pearson, Murray ni mchezaji wa pili kujiondoa katika kipindi cha siku mbili zilizopita, kwani Rafael Nadal wa Hispania aliandika barua ya kujiondoa kwa madai kuwa anajiandaa na michuano ya wazi ya Australia.

0 comments:
Post a Comment