Wednesday, 3 January 2018

Tanzania yateuliwa kuandaa mkutano mkuu wa mwaka FIFA



Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA utakaofanyika February 22, 2018 jijini  Dar es Salaam na ikishirikisha mataifa 19 wanachama wa FIFA na mwenyekiti wa mkutano huo akiwa ni Rais wa FIFA Gianni Infantino. Miongoni mwa agenda zitakazojadiliwa ni pamoja na utoaji wa fedha za FIFA kwa ajili ya maendeleo ya soka, kutafuta suluhu ya changamoto za usajili kwa njia ya mtandao, Transfer Matching System (TMS).
Rais wa TFF Wallace Karia wakati akitangaza kufanyika kwa mkutano huo amesema, ni heshima kwa Tanzania na TFF kuwa mwenyeji wa mkutano huo mkubwa wa shirikisho la soka Duniani.
Mataifa yatakayoshiriki mkutano huo ni Tanzania (mwenyeji), Algeria, Mali, Morocco, Burkinafaso, Angola, Niger, Bahrain, Palestina na Saud Arabia.
Mengine ni Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Tunisia, Bermuda, Monserrat, St Lucia, Visiwa vya US Virgin, Maldives na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

0 comments:

Post a Comment