Tuesday 16 January 2018

Waziri Mkuu Somalia aiomba jumuiya ya kimataifa kuleta utulivu



Waziri mkuu wa Somalia Bw. Hassan Ali Khaire amesisitiza jumuiya ya kimataifa iunge mkono serikali ya Somalia kuanzisha mchakato wa mageuzi kwa idara za usalama za nchi hiyo.
Bw. Khaire aliyeendesha mkutano wa mageuzi ya idara za usalama mjini Mogadishu, amesema Somalia bado inahitaji tume ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Afrika AMISOM kusaidia kulinda utulivu.
AMISOM imeahidi kuendelea kuunga mkono mchakato wa mpito kwenye majukumu muhimu, zikiwemo kuhakikisha njia kuu za ugavi, kulinda usalama wa maeneo yenye watu wengi, na kutoa mafunzo na misaada kwa idara za usalama za Somalia zikiwemo jeshi na polisi, kwa kushirikiana na tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia na kuendana na mipango ya usalama ya kitaifa.

0 comments:

Post a Comment