Saturday 17 March 2018

Mwanasheria mkuu Marekani amtimua kazi Naibu Mkurugenzi FBI



Mwanasheria Mkuu nchini Marekani, Jeff Sessions amtimua kazi Naibu Mkurugenzi wa FBI, Andrew McCabe ambaye alibakiza siku 2 kabla ya kustaafu

McCabe alishika wadhifa huo mara baada ya Rais Trump kumtimua kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa FBI, James Comey mnamo Mei 9 mwaka jana(2017).

Katita taarifa ya kumfuta kazi, Jeff Session amesema kuwa McCabe hakuwa mkweli na alivujisha taarifa kwa Wanahabari na aliwapotosha wachunguzi wakati wakifuatilia tuhuma dhidi yake
Ikumbukwe kuwa McCabe alihusika kwa kiasi kikubwa katika kuchunguza tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi Mkuu wa Marekani pamoja na sakata la barua pepe za Bi. Hillary Clinton
Mapema leo Rais Trump kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameandika kwa furaha kuwa '' Andrew McCabe amefukuzwa kazi, ni siku nzuri sana kwa wachapakazi wote Wanaume kwa Wanawake ndani ya FBI, ni siku nzuri kwa Demokrasia. Na kumtuhumu kuwa alikuwa akijua kila uovu uliokuwa ukiendelea ndani ya FBI



Kwa upende wake McCabe amesema kuwa amefanyiwa yote hayo kutokana na mchango wake alioutoa baada ya kufutwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa FBI, James Comey

0 comments:

Post a Comment