Thursday 15 March 2018

Theresa May kuwatimua wanadiplomasia wa Urusi



Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amewapa muda wa wiki 1 Wanadiplomasia 23 wa Urusi kuondoka nchini humo baada ya kushindwa kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa shambulio la sumu iliyotengenezwa na taifa lao na kutumika kumshambulia Afisa Usalama wa zamani wa Urusi, Sergei Skripal na Binti yake Yulia

Hata hivyo Serikali ya Urusi imekana kuhusika na mpango wa mauaji ya wawili hao. Bwana Sergei Skripal alikuwa Afisa Usalama wa Jeshi la Urusi lakini pia aliwahi kufanya kazi na Shirika la Usalama la Uingereza kuanzia miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000

Mwaka 2004 alikamatwa na Shirika la Usalama la Urusi akituhumiwa kwa makosa mbalimbali likiwemo kosa la Uhaini na baada ya kuachiwa huru mwaka 2010 aliamua kuweka makazi yake nchini Uingereza katika Mji wa Salisbury

Machi 4 mwaka huu yeye pamoja na Binti yake Yulia(Aliyewasili kutoka Urusi) walishambuliwa kwa sumu kali ilitotengenezwa nchini Urusi na hadi sasa wamelazwa hospitali wakiwa katika hali mahututi

0 comments:

Post a Comment