Friday 6 April 2018

Black Panther yaandika historia mpya Duniani



Filamu mashuhuri zaidi duniani kwa sasa, Black Panther, inaandika historia nyingine baada ya kupewa kibali cha kuwa filamu ya kwanza kuoneshwa hadharani nchini Saudia Arabia kufuatia zuio la maonesho ya filamu lililodumu kwa takribani miaka 35
-
Filamu hiyo itaoneshwa Aprili 18, 2018 katika ukumbi mkubwa wa kitaifa wa cinema ambao ulifunguliwa Desemba, 2017 baada ya Mwana wa Mfalme, Mohammed Salman kutangaza kufuta zuio hilo
-
Kuanzia miaka ya 1980's, Saudia Arabia ilipiga marufuku maonesho ya filamu kwa madai kwamba filamu nyingi hazina maadili ya kiislamu na zinatumika kueneza tamaduni za nchi za magharibi hivyo kudhoofisha tamaduni asilia za nchi hiyo
-
Hata hivyo, kutokana na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi yanayofanywa na Serikali iliyopo madarakani kwa dhamira ya Mwana wa Mfalme, Mohammed Bin Salman, kuanzia mwaka 2017 mazuio mengi yaliyopitishwa na wahafidhina wa nchi hiyo yameanza kuondolewa ili Saudi Arabia iendane na kasi ya dunia kwenye masuala ya kiuchumi na kijamii kwa ujumla

0 comments:

Post a Comment