Michuano ya robo fainali ya ligi
ya Europa imepigwa jana kwa michezo minne. Arsenal imeichapa bila huruma
CSKA Moscow magoli 4-1, dakika 26 kabla ya mapumziko, Alexandre
Lacazette na Aaron Ramsey waliifungia Arsenal magoli mawili. Katika
kipindi vcha pili dakika za 28 na 35 wachezaji hao walishindilia karamu
ya magoli kwa kuongeza magoli mawili mengine. Hadi mwisho wa mchezo
Arsenal iliibuka kidedea kwa ushindi huo mnono.
Michezo mingine ilikuwa kati ya Atletico Madrid imeifunga Sporting
Lisbon magoli 2-0, nayo Lazio imeicharaza RB Salzburg magoli 4-2 huku RB
Leipzig imeifunga Marseille 1-0.
0 comments:
Post a Comment