Wizara ya afya ya umma ya
Afghanistan imesema mlipuko uliotokea jana karibu na kituo cha
kuandikisha wapiga kura mjini Kabul, umesababisha vifo vya watu 57 na
wengine 119 kujeruhiwa. Kwa mujibu wa wizara hiyo, wengi wa waliouawa ni
raia wa kawaida, wakiwemo wanawake 21 na watoto watano, na kundi la
Islamic State limetangaza kuwajibika na shambulizi hilo. Imefahamika
kuwa uchaguzi wa bunge nchini Afghanistan utafanyika Oktoba 20 mwaka
huu, na kazi ya kuandikisha wapiga kura imeanza Aprili 14 kote nchini
humo.
0 comments:
Post a Comment