Saturday 7 April 2018

Mbunge ahoji mamlaka ya Bakwata



Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji amehoji Serikali inatumia vigezo gani au sheria ipi kuitambua BAKWATA kwamba ndio Baraza Kuu na chombo kikuu cha kuwasemea Waislamu?

Amesema jambo hilo halipo kwenye Kitabu kitukufu cha Quran, Quran haitambui BAKWATA wala Uhamsho inatambua Uislamu na Imani ya Kiislamu

Amedai Waislamu wana taasisi nyingi ambazo kwa mujibu wa sheria za Kiislamu si juu ya Serikali kuingilia. Kila Muislamu na maamuzi na tasisi na jumuia anayoiona

Amedai Serikali imeendelea kuitambua BAKWATA na kupia majukumu makubwa ikiwemo kusimamia hija za Waislamu, kusimamia mashtaka ya Waislam, jambo ambalo si haki. Pia ameitaka Serikali kuacha kufanya hivyo

0 comments:

Post a Comment