Serikali imemkabidhi Bendera ya Taifa muigizaji wa filamu, Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana kuwania tuzo ya The African Prestigious Award kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika
Monalisa ndiye msanii pekee kutoka Tanzania aliyeteuliwa kuwania tuzo hizo zenye heshima kubwa ambazo zitafanyika hivi karibuni huko Accra, Ghana.
Tuzo hizo hutolewa kwa kutambua maendeleo na tija aliyonayo mtu kwenye nyanja za uongozi, biashara, sanaa na kadhalika.
0 comments:
Post a Comment