Friday, 27 April 2018

Sheria mpya za IAAF kuwaathiri wanariadha wakike wenye uwezo kama wanaume



Sheria mpya za chama cha riadha duniani (IAAF) ambazo zitaanza kutumika Novemba mosi mwaka huu, zitawahusu wanariadha wa kike wanaokimbia kuanzia mita 400 hadi maili moja. Sheria hizo zinawataka baadhi ya wanariadha wa kike wenye homoni nyingi za kiume watatakiwa kukimbia dhidi ya wanaume au kubadili mashindano hadi pale watakapopata matibabu.
Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya ambaye ni mshindi wa mita 800 kwenye michuano ya Olimpiki amesema yupo tayari kukimbia umbali mrefu zaidi.

0 comments:

Post a Comment