Wednesday 23 May 2018

Dawa za kulevya zamponza Bondia Marekani


Bondia Eric Molina wa Marekani amepewa adhabu ya kutoshiriki mchezo wa masumbwi kwa muda wa miaka miwili baada ya vipimo kuonyesha kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu michezoni katika pambano lake la Disemba mwaka 2016 alipopigana na Anthony Joshua wa Uingereza.

Akipokea adhabu hiyo, Eric mwenye miaka 36, hakukana kosa hilo, lakini alichohoji ni ukubwa wa kifungo chake, akizitaka mamlaka zinazohusika kutafakari.

Hata hivyo kwenye pambano hilo alilotumia dawa zilizokatazwa aliangushwa kwenye raundi 5 na AJ ambaye wakati huo alikuwa anatetea mkanda wake wa IBF.

0 comments:

Post a Comment