Serikali imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp baada ya kuwepo kwa jumbe kadhaa zilizosambazwa na kuleta vurugu katika jamii
Katika kupambana na hali hiyo WhatsApp imetangaza kuzuia uwezo wa kusambaza ujumbe(Forwarding Message) kwa watumiaji wake takribani milioni 200 nchini humo
WhatsApp imesema itazuia uwezo wa kusambaza ujumbe na kuwafanya watumiaji wake waweze kusambaza ujumbe kwa makundi au watu wengine watano tu(5 chats)
Tangu mwisho wa mwezi wa nne, zaidi ya watu 20 wameuawa kwa kupigwa na makundi ya watu kwa ktuhumumiwa kuteka na kubaka watoto ambapo taarifa hizi zilikuwa zikisambazwa kupitia WhatsApp
Aidha, takribani watu 32 ikiwemo viongozi wa makundi ya WhatsApp(Administrator) ambayo yanahusika katika kusambaza habari hizo za uongo wamekamatwa
0 comments:
Post a Comment