Wednesday, 3 January 2018























Magazeti ya leo Jumatano 3/1/2018

Tuesday, 2 January 2018

California limekuwa jimbo kubwa zaidi nchini Marekani kuhalalisha matumizi ya bangi kwa burudani.

Kuanzia sasa Januari mosi mwaka 2018 watu walio na umri wa kuanzia miaka 21, wanaweza kumiliki hadi gramu 28 za bangi na kupanda hadi miti 6 ya bangi nyumbani.
Wanaopinga wanasema kuwa sheria hiyo itasababisha watu kuendesha magari wakiwa tayari wamevuta bangi kuchangia vijana kuvuta bangi.
Lakini biashara zinatabiri kile kinaonekana kuwa sekta ya mabilioni ya dola miaka michache inayokuja.
Wakaazi wa Califonria walipigaa kura kuunga mkono kipengee cha kuhalalisha bangi miaka 14 iliyopita katika kura ambayo ilifanyika sambamba na uchaguzi wa rais nchini humo.
Tangu wakati huo sheria ngumu zinazohusu kodi zimeandikwa kudhibiti mauzo ya bangi.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ambayo inafuatilia soko la bangi duniani alitabiri kuwa kutakuwa na kushuka kwa bei kwa mwaka wa kwanza au miaka miwili.
Hata hivyo, faida ni kubwa katika jimbo hilo tajiri zaidi na lenye watu wengi zaidi nchini Marekani.
Mwaka 1996, California lilikuw jimbo la kwanza kuhalalisha bangi kwa matumizi ya matibabu.
Inakadiriwa kuwa soko la bangi haramu kwa sasa ni dola milioni 5.1 na wakati itahalalishwa thamani yake itakuwa ya dola bilioni 5.8 itakapofikia mwaka 2021.

Matumizi ya bangi yahalalishwa California


King Kaka – Mistarillionaire


Rais John Magufuli akitia saini kitabu cha maombelezo nyumbani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Kangi Alphaxard Lugola aliyefiwa na mkewe Mary Lugola asubuhi taehe 1-1-2018.

Rais Magufuli azuru msiba wa mke wa Naibu Waziri, Kangi Alphaxard Lugola


China imeidhinisha rasmi sheria ya kupiga marufuku uuzwaji na uchakataji wa aina yoyote wa bidhaa zitokanazo na pembe za wanyama nchini humo.

Balozi wa Kampeni ya kimataifa ya kuzuia ujangili husuani wa Tembo duniani (WILDAD), Yao Ming, ambaye ni Mchezaji wa zamani wa ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani NBA, ikiwajumuisha pia David Beckham, Leonardo Dicaprio, Prince William, Ali Kiba, JackieChan, na wengineo, amesema hatua hiyo ni kubwa kwa serikali ya China.

China ambayo ni moja ya soko kubwa la Pembe za Ndovu kutoka Afrika na duniani, mnamo mwaka 2016 ilitangaza kuwa ifikapo mwisho wa mwaka 2017 itapitisha sheria kukomesha biashara hiyo nchini mwake.

Sheria hiyo inakomesha pia biashara ya mtandao na kwa atakayekutwa na hatia anakabiliwa na kifungo cha miaka kumi mpaka maisha jela.

Uhitaji wa pembe hizo katika soko la ndani la China, umeripotiwa kuchochea ujangili dhidi ya Tembo hususani katika nchi za Tanzania na Kenya.

China yapiga marufuku uuzwaji bidhaa zitokanazo na pembe za wanyama


Katibu wa Itikadi na Uenezi  wa  Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole amemtahadharisha Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwakumwambia kuwa  kipindi hiki ni cha mwisho kuongoza Jimbo hilo la Arusha Mjini.

Hayo yamekuja mara baada ya Mbunge huyo kupitia kurasa zake za twitter kujibizana huku Lema akionyesha kumhoji Polepole kama familia yake huwa inamuelewa kweli anachokizungumza.

“Term ya mwisho Arusha, tunataka Mbunge wa Masuala na si wa Matukio, hata mkichezesha draft ili uende Hai, haitawezekana maana hata “fly to…” maji yako shingoni, na ukiamua kurudia kazi yako ya zamani. anko Siro is very serious,”ameandika Polepole

Polepole,Lema watunishiana misuli Tweeter


CNN  wamesema kuwa Uongozi wa Donald Trump umefanya wasanii wengi zaidi nchini Marekani kutunga nyimbo zenye kupinga uongozi wake tangu aingie madarakani mwaka 2017.

Kituo hichi kikubwa cha habari kinasema kumekuwa na muongezeko wa kazi za Conscious Rap kutoka kwa wasanii wakubwa Marekani huku jamii ikiziunga mkono kazi za sanaa na kuonyesha kutaka kusikilizwa kwa hoja zao na hitaji la mabadiliko kwa jamii ya watu weusi nchini Marekani.
Wasanii ambao wamo katika oodha ya  CNN ni pamoja na,
  •  Jay-Z >Kupitia album yake ya 4:44 katika nyimbo kama “The Story of O.J.”
  •  Eminem> Alifanya free style kali kumpinga Donald Trump na kusema hataki kuwa na mashabiki wanaounga mkono Serikali yake katika tuzo za HipHop za BET
  •  Kendrick Lamar
  • Rapsody
  •  Joey Bada$$
  •  J. Cole
  •  Vic Mensa

CNN yasema uongozi wa Trump umefanya wasanii Marekani kuimba siasa

Manchester United wamefanikiwa kurejea katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya uingereza baada ya kuwafunga Evertonkwa magoli 2-0.

Magoli ya United katika mechi hiyo yalifungwa na Anthony Martial kunako dakika ya 57 na goli la pili likifungwa na Jesse Lingard katika dakika ya 81.
Katika matokeo ya mechi nyingine iliyofanyika jana Liverpool imeendeleza wimbi la ushindi ilipowafunga Burnley kwa magoli 2-1 na magoli yao yakifungwa na Sadio Mane na Ragnar Klavan , huku goli pekee la Burnley likifungwa na Johann Gudmundsson.
Sasa Manchester United wanasubiria matokeo ya mchezo kati ya Arsenal na Chelsea utakaopigwa siku ya Jumatano ambapo kama Chelsea atafungwa watabaki nafasi ya pili lakini Chelsea akishinda United watarudi katika nafasi ya tatu .

Manchester United yarudi kileleni

 

Mchezaji namba moja kwa viwango vya ubora wa Tennis kwa upande wa wanawake, Simona Halep wa Romania ameanza vizuri msimu mpya wa mashindano kufuatia ushindi mnono wa seti ya 6-4 6-1 alipocheza dhidi ya Nicole Gibbs wa marekani kwenye Mashindano ya wazi ya Shenzhen yalioanza jana katika jimbo la Guangdong hapa China.

Huu ni mwanzo mzuri mchezaji huyo amabye anajiandaa pia na mashindano ya Australia yanayotarajiwa wiki mbili zijazo akiwa nimiongoni mwa wanaopewa nafasi ya kutwaa ubingwa.
Katika michezo mingine iliyofanyika jana, Maria Sharapova wa Urusi, naye alipata ushindi katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Mihaela Buzarnescu kwa seti ya 6-6 6-0.

Halep na Sharapova waanza mwaka kwa ushindi-Tennis


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana wanaioishi kwenye mikoa ambayo zao la korosho linastawi wachangamkie kilimo cha zao hilo kwa sababu lina fursa nyingi.

“Mahitaji ya korosho ni makubwa duniani, korosho zinatumika mahotelini na kwenye mikutano mikubwa, zinatumika kwenye ndege, kwa hiyo bei yake lazima iwe kubwa,” alisema.

Ametoa wito huo Jumapili, Desemba 31, 2017 wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Kaulimbiu ya kampeni hiyo ni: “Korosho ni dhahabu ya kijani, tuitunze, itutunze”.

Waziri Mkuu alisema anaamini kuwa kijana yoyote mwenye nguvu ya kufanya kazi hawezi kushindwa kulima zao hilo kwa sababu halihitaji uangalizi mkubwa. “Kijana yeyote anaweza kulima zao hili kwa sababu ekari moja ina miche 37 hadi 40. Kuna mtu atashindwa kuangalia miche 37 hadi ikue?” aliuliza.

Waziri Mkuu alisema kilimo cha korosho ni rahisi lakini pia kilimo cha korosho ni rafiki wa mazingira, kwani miti ikikua inatunza mazingira na inasaidia kuleta mvua. Alisema mbali ya mikoa inayolima korosho ya Lindi, Mtwara, Ruvuma Pwani na Tanga, kuna mikoa mingine ambayo udongo wake umepimwa na kubainika kuwa zao hilo linaweza kustawi bila shida.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, Kigoma, Njombe, Songwe na kuongeza kuwa mikoa ya Singida na Manyara iko mbioni kukamilisha uchunguzi wake.

“Leo tumeanza usambazaji wa miche ya bure hapa Ruangwa ambao najua utafuatiwa na wilaya nyingine hapa nchini. Nimeelezwa kwamba mche wenye kutoa mazao mengi ni wa kuanzia miaka mitatu hadi saba, kwa umri huu miche ya korosho inaweza kuchanganywa na mazao mengine kama ambavyo mtashauriwa na maafisa kilimo ili wakati wa palizi ya hayo mazao, shamba lako la korosho libakie kuwa safi,” alisema.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka jimboni kwake.

Mapema, akitoa taarifa ya taarifa ya uzalishaji wa miche ya mikorosho msimu wa 2017/18 mkoani Lindi, Katibu Tawala wa mkoa huo, Bw. Ramadhani Kaswa alimweleza Waziri Mkuu kwamba katika msimu wa 2016/2017, mkoa huo uliweka lengo la kuzalisha na kupanda miche 1,000,000 ya mikorosho.

“Hadi mwisho wa msimu huu, jumla miche 716,532 ilizalishwa na kusambazwa kwa wakulima sawa na asilimia 71.6 ya lengo lililowekwa. Kati ya hiyo, Halmashauri ya Kilwa ilizalisha miche 55,000, Halmashauri ya Lindi miche 100,000, Manispaa ya Lindi miche 50,000; Halmashauri ya Liwale miche 106,000; Halmashauri ya Nachingwea miche 227,670 na halmashauri ya Ruangwa miche 177,862,” alisema.

“Miche hii iligawanywa kwa wakulima bure ambao walipanda kwenye mashamba yao. Zoezi la tathmini ya miche iliyokua baada ya kupandwa linaendelea kwenye halmashauri zote za mkoa,” aliongeza.

Bw. Kaswa alisema kutofikiwa kwa lengo hilo kumechangiwa na kutopatikana kwa mahitaji yote ya mbegu na vifaa vya uzalishaji, kuchelewa kwa vifaa, na mwamko mdogo wa vikundi vya uzalishaji.

Alisema kwa msimu huu wa 2017/2018, mkoa uliweka lengo la kuzalisha miche ya mikorosho iliyobebeshwa na isiyobebeshwa 7,132,000. Kati ya hiyo, Wilaya ya Kilwa walilenga miche 1,122,000, Lindi Vijijini 1,550,000, manispaa ya Lindi 1,000,000, Liwale miche 450,000, Nachingwea miche 1,810,000 na Ruangwa miche 1,200,000.

“Hadi kufikia tarehe 29 Desemba, 2017 tayari miche 4,974,425 ilikuwa imezalishwa na iko tayari kwa kupandwa kwenye mamlaka za serikali za mitaa kama ifuatavyo:- Kilwa miche 772,000, Lindi Vijijini 1,160,455, manispaa ya Lindi 771,440, Liwale miche 266,000, Nachingwea 991,070 na halmashuri ya Ruangwa imezalisha miche 1,013,460,” alisema.

Sherehe hizo za uzinduzi wa upandaji miche mipya zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya, baadhi ya Wenyeviti wa Halmashauri na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele walishiriki uzinduzi huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mkuu awaasa vijana kulima korosho


Mwandishi wa Habari za vikaragosi/Vikatuni nchini Tanzania, Masoud Kipanya amejitokeza hadharani baada ya taarifa za kushikiliwa na  kusambaa mitandaoni jana Januari 01, 2018 taarifa  kuwa Masoud Kipanya amekamatwa na watu wasiojulikana ambapo hata kampuni ya Clouds Media Groups ilishindwa kutolea maelezo ya kina ya taarifa hizo.

Kipanya amethibitisha taarifa hizo za kupatikana kwake kupitia kurasa zake za mitanda ya kijamii ameandika kuwa anamshukuru sana mtu aliyesambaza taarifa za kukamatwa kwani ndio zimemuokoa.
Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine. Niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa. ‘AMESAIDIA’.“ameandika Masoud Kipanya.

Masoud Kipanya ajitokeza hadharani,Amshukuru aliyesambaza taarifa za kupotea kwake


Habari Zilizopo ndani Magazeti ya Leo Jumanne ya January 2

Monday, 1 January 2018

Staa wa kikapu nchini Marekani anayekipiga katika timu ya Hauston Rocket,James Harden ameonesha upendo wa dhati kwa rafiki wake wa muda mrefu Meek  Mill baada ya kutengeneza kiatu  chenye maandishi yanayotaka kuachiwa kwa msanii huyo anayehudumu kifungu cha miaka miwili FREE MEEK na kuvivaa kwenye mchezo wao dhidi ya Boston Celtics
James amesema Meek Mill yuko sawa, tuna matumaini ya kumtoa February 2018, ana mpango wa kutoa muziki mpya akirudi nyumbani.

 

James Harden atengeneza kiatu kwaajii ya Meek Mill(Free Meek)


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Kangi Lugola amefiwa na mkewe Mary.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Mary amefariki dunia leo Jumatatu Januari Mosi, 2018 jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa utaratibu wa mazishi unaendelea kufanyika na taarifa zitatolewa baadaye.

Wakati huohuo, Ofisi ya Bunge katika taarifa kwa umma imesema Spika Job Ndugai amemtumia rambirambi Lugola kutokana na kifo cha mkewe.

Imeelezwa msiba upo Railway Club Gerezani jijini Dar es Salaam.

Ndugai ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao.

TANZIA-Mke wa Naibu Waziri, Kangi Lugola afariki dunia leo

Wanaitwa Gidion na Joshua. Ni kazi yao ya kwanza kufanya cover ya Namba moja ya kwake Paul Clement. Kazi imefanyika Fisher Records

Paul Clement awapa nafasi Gidion,Joshua kufanya cover 'Namba Moja'

Mwanamuziki wa Bongo Hakeem Bamuyu akiwa ameshirikiana na Barakah The Prince wameachia video ya wimbo mpya wa Ungeniambia. Audio imetengezwa na Shedy Clever na Video imeongozwa na Joowzey.

New Music Video: Hakeem Bamuyu Ft Barakah The Prince – Ungeniambia

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mjumbe wa kamati kuu wa  Chadema ,Mhe. Edward Lowassa amewaasa Watanzania mwaka 2018 wakatae kugawanywa kwa namna yoyote ile na wawe na ushirikiano. Lowassa kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika hayo na kuwatakia Watanzania kheri ya mwaka mpya wa 2018.

Tunapouanza mwaka huu mpya niwaombe watanzania wenzangu tukatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile.“ameandika Mhe. Lowassa na kuwatakia Watanzania kheri ya mwaka mpya “Umoja na mshikamano ndio nguzo yetu. Nawatakia Heri na Fanaka ya mwaka mpya 2018.

Lowassa awaasa watanzania kuwa na ushirikiano mwaka 2018


Fid Q Ft. Diamond Platnumz & Rayvanny – Fresh Remix

Moto mkubwa umeharibu karibu magari 1,400 kwenye jengo la ghorofa la kuegesha magari huko Liverpool na kuwalazimu watu wengi kuukaribisha mwaka kwenye makao ya muda.

Wazima moto walisema kuwa moto huo katika jengo la King's Dock karibu na ukumbi wa Liverpool Echo Arena, ni mioto mibaya zaidi kuwai kukabiliana nayo

Polisi walisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa moto kutoka kwa gari ulisambaa kwenda kwa mengine.
Watu walihamishwa kutoka majengo yalito karibu kutokana na moshi.
Polisi wa Merseyside walisema kuwa magari ya kuzima moto 21 yalikuwa eneo hilo na huma za wazima moto zilesema zilikuwa zinachukua tahadhari ya jengo hilo kuporomoka.
Magari yote yaliyokuwa kwenye jengo hilo linaloweza kuegeshwa magari 1600 yaliharibiwa. kwa mujibu wa polisi.
Waliwashauri watu kubaki manyumbani mwao na kufunga madirisha ikiwa wangeona moshi kutoka kwa moto huo.

Moto wateketeza Magari 1,400 Liverpool,Uingereza

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa na kibonyezo cha silaha za nyuklia kwenye meza yake wakati wote na hivyo Marekani isithubutu kuanza vita.

Katika hotuba ya mwaka mpya iliyopeperushwa kwa njia ya runinga, alisema kuwa Marekani inaweza kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskania akiongeza kuwa huo ni kweli na wala sio vitisho.
Lakini pia alitoa wito kwa Korea Kusini kuja kwenye mazungumzo.
Korea Kaskazini pia itatuma kikosi katika mashindano ya olimpiki ya msikmu wa baridi nchini Korea Kusini, Kim alisema.
Wakati aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu vitisho vya Kim, Rais wa Marekani alisema, "tutaona, tutaona".
Alikuwa akizungumza kando mwa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya katika eneo lake ya kifahari la Mar-a-Lago huko Florida.
Korea Kaskazini imewekewa vikwazo zaidi mwaka uliopita kwa kutokana na mipango yake ya silaha za nyuklia na majaribio ya mara kwa mara ya silaha hizo.
Taifa hilo lililotemgwa lilifanya majaribio 6 ya nyuklia ya chini ya ardhi na kuonyesha kuongeza uwo wake wa makombora
Mwezi Novemba ilifanyia majaribio kombora lake la Hwasong-15 ambalo lilipaa umbali wa kilomita 4,475 mara kumi zaidi kuliko kituo cha safari za anga za juu.

Kim Jong-un kuanza vitisho siku ya mwaka mpya


 

Mchezaji Manchester United Ashley Young afungiwa na kulazimika kutocheza mechi tatu mfululizo baada ya kufungiwa na chama cha soka FA.

FA imemfungia mchezaji huyo  kufuatia kitendo chake cha kumpiga kwa kiwiko cha mkono Dusan Tadic wa Southampton katika mechi baina ya timu hizo mbili iliyoisha kwa sare ya kutofungana jumamosi iliyopita.
Tukio hilo halikuonwa na moja kwa moja na mwamuzi, lakini kamera za uwanjani hapo zilimnasa na kwa mujibu wa kanuni za FA analazimika kufungiwa.
Kutokana na adhabu hiyo, Young atakosa mechi ya ligi kuu leo dhidi ya Everton, pia mechi dhidi ya Derby County ya kombe la FA pamoja na mechi nyingine ligi kuu dhidi ya Stoke City

Ashley Young wa Manchester United aanza mwaka na kufungiwa

 

Bondia Muingereza Anthony Joshua ambaye ni bingwa wa uzito wa juu duniani kwa sasa akishikilia mikanda mitatu mikubwa amesema hatoendelea kumheshimu bondia Tyson Fury licha ya mafanikio aliyowahi kuyapata.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye mahijoano maalum aliyofanya jana, akisisitiza amefikia uamuzi huo kutokana na kile alikiita kuwa ni dharau za wazi anazofanya Fury dhidi yake na kumvunjia heshma kila kukicha.
Fury ambaye ni mwingereza pia, mara kadhaa amekaririwa akibeza ushindi anaoupata Joshua na akitaka jamii iache kumpongeza kwani hajafikia viwango vya ubora.
Katika mahojiano hayo Joshua mwenye mikanda ya ubingwa wa WBA, IBO na IBF alizungumzia ujio wa pambano lake dhidi ya Joseph Parker litakalofanyika mwezi machi mwaka huu.

Anthony Joshua amtolea uvivu Tyson Fury


Happy new year 2018 song


Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amewataka Watanzania kuwa tayari kukosolewa na viongozi wa dini kwani ndio wanaoliombea Taifa liwe na amani katika kipindi chote tangu nchi ilipopata Uhuru.

Mbowe ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu hali ya kisiasa kwa mwaka 2017, ambapo alisema kila mtu ana mapungufu katika utendaji wake wa kazi hivyo kila mmoja awe tayari kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini.

“Lakini viongozi wetu wa dini wana haki ya kusema, wana wajibu wa kusema, hawa ni watu wanaolea Taifa hili kiroho, huwezi kumshambulia Kakobe kama unamshambulia mtoto mdogo, hawa wana waumini wana followers (wafuasi) na hawa ndio kila siku Rais anasema wamwombee, sasa wanamwombea vipi wakati unawapa masharti?,” alisema Mbowe na kuongeza.

“Sisi wapinzani tunakosolewa, viongozi tuwe na unyenyekevu wa kukubali mawazo tofauti tukisemwa, tusijenge chuki katika jamii, vyama vyetu vyote vinaongozwa na binadamu vinaweza vikakosea, tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao, tukikosea waseme.”

Chadema yamaliza mwaka na hili