Kwa mara ya kwanza katika
historia ya soka ya Ligi Kuu ya Uhispania, pambano la El Clasico kati ya
Real Madrid na Barcelona litasakatwa mchana.
Kwa mujibu wa waandaaji, kipute hicho cha kesho Jumamosi kitaanza saa tisa alasiri ili kutoa fursa kwa mashabiki wa bara Asia kushabikia klabu hizo maarufu. Kulingana na utafiti wa La Liga, mashabiki wapatao milioni 650 watashuhudia pambano hilo kutokana na umaarufu wa klabu hizo, upinzani mkali wa miaka mingi na tofauti za kisiasa baina ya timu hizo kutokana na utamaduni wa miji yao ya Catalonia na Madrid.
Mechi hiyo ya kesho itachezwa saa tisa alasiri ili ishuhudiwe na mashabiki wengi wa miji ya Shangai, Jakarta, New Delhi na miji mingine ya bara Asia. Kulingana na utafiti uliofanywa na Nielsen Sports, La Liga Clasico ya kwanza msimu uliopita ilifaidisha vyombo vya habari kwa kiasi cha Sh68 bilioni kupitia matangazo ya wadhamini.

0 comments:
Post a Comment