Thursday 18 January 2018

Teknolojia ya China kutumika katika sensa Ethiopia

Shirika la takwimu la Ethiopia limesema kuwa tablet 180,000 zilizonunuliwa kutoka kwa makampuni ya teknolojia ya habari na mawasiliano ya China, Huawei na Lenovo, zitatumika katika sensa ya nne ya nyumba na idadi ya watu nchini Ethiopia. 

 

Shirika hilo limedokeza kuwa tablet hizo zimefanyiwa majaribio na kuidhibishwa na idara hiyo. Kwa mara ya kwanza Ethiopia itatumia utaratibu wa kisasa kwenye sensa ya nyumba na idadi ya watu.
Makampuni hayo ya China yamekubali kutoa tablet zitakazotumika katika mchakato wa kujiandikisha.
Kwa mujibu wa wataalamu wa Shirika la Takwimu la Ethiopia, matumizi ya tablet hizo kwenye sensa, yatapunguza ugumu wa kazi ya kukusanya data na kuondoa dosari ya kuhesabu mara mbili.

0 comments:

Post a Comment