Thursday 18 January 2018

Sudan yaitunuku ripoti ya UN kuhusu kukusanya silaha Darfur



Serikali ya Sudan imepongeza ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, inayosisitiza kuwa mpango wa serikali ya Sudan wa kukusanya silaha katika eneo la Darfur utahimiza usalama kwenye eneo hilo.
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imetoa taarifa ikipongeza ripoti iliyotolewa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, inayotambua utulivu katika eneo la Darfur. Taarifa hiyo imesema kampeni ya kukusanya silaha inayoongozwa na serikali ya Sudan imeleta utulivu, na kusaidia kuimarisha amani na usalama katika eneo la Darfur, na kusisitiza kuwa serikali ya Sudan itaendeleza ushirikiano na uratibu kati yake na tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika eneo la Darfur UNAMID.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres ametoa ripoti kwa Baraza la usalama la UN akipongeza kampeni hiyo ya kukusanya silaha, ambayo inatakiwa kuendelea kufanyika kwa kufuata makubaliano ya Doha kuhusu amani katika jimbo la Darfur.

0 comments:

Post a Comment