Mgahawa maarufu kwa kuuza kuku na 'chipsi' wa KFC, nchini Uingereza umelazimika kufunga matawi yake zaidi ya 600 nchini humo baada ya kukosa kuku katika kipindi cha mwezi sasa.
Taarifa iliyotangazwa na uongozi wa KFC imeeleza kufuatia upungufu mkubwa wa Kuku, wamelazimika kupunguza wafanyakazi na kuwaomba wengine kuacha kazi kwa hiari
"Hatuna uhakika lini kuku wa kutosha watapatikana, ni vyema tukafunga na kujipanga upya," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo. Uingereza ina jumla ya matawi 900 ya KFC
KFC ambayo pia ina matawi nchi mbalimbali duniani, Tanzania ikiwamo, inatarajia kuagiza kuku kutoka nje ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment