Saturday 3 February 2018

TUKUTANE KYIV.


Na Raphael Mwenda.
      Mbio za ubingwa pale uingereza zinaonekana kuisha huku Manchester city ikipewa nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa huo kule Hispania Barcelona nae amejiweka katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa huo achilia mbali Ufaransa na Ujerumani ambako mabingwa wamezoeleka. Kwasasa macho na matamanio yote yapo katika kuifata ile njia ienday Ukraine katika jiji la Kyiv.
            Fainali ya ligi ya mabingwa ulaya itachezwa katika uwanja wa NSC Olimpiyskiy Stadium pale Kyiv Mnamo mwezi may mwaka huu. Baada ya ligi zote kubwa mabingwa kuanza kuonekana wazi mbio za kuelekea Kyiv zimeongezeka utamu maradufu. Je Zizzou ataondoka mikono mitupu msimu huu? Antonio Conte nae itakuaje pale Stanford bridge? Jurgen Klopp atakua bado anatengeneza timu kule anfield? Jose Mourinho pale old trafford hali itakuaje? Massimiliano Allegri kule Turin mambo yatakuaje? Mauricio Pochettino nae ataendelea kuwa msindikizaji? Hawa makocha wote mpaka sasa hakuna mwenye uhakika na kikombe. Tuzitazame timu hizi kabla ya kuelekea Kyiv.
        REAL MADRID : Hawajawa na msimu mzuri sana mwaka huu kutokana na matatizo ya hapa na pale hasa katika dirisha la usajili mwezi juni mwaka jana baada ya kushindwa kukidhi matakwa ya mwalimu. Wamekwisha ondolewa katika kombe la mfalme na wameachwa pointi 19 na vinara Fc Barcelona si kitu rahisi kwasasa kwa wao kuchukua ubingwa wa la liga nguvu na matamanio yao yote kwasasa ni kuchukua ubingwa wa ulaya kwa mara ya tatu mfululizo, mbele yao yupo PSG katika ubora wake je watafanikiwa kusogea kituoni kusubiri gari la kuelekea Kyiv?
           JUVENTUS : Bado ni mapema sana kuwatoa katika mbio za ubingwa pale Italy kwani wameachwa pointi moja tu na vinara SSC Napoli. Baada ya Leonardo Bunocci kuondoka ukuta wao kidogo umeyumba japo wamejaribu kuingiza wachezaji wengine kama Benedikt Howedes kutoka kule Schalke 04 na Benatia ambae alikuepo pale kwa kipindi fulani. Giorgio Chiellini umri umekwenda Bazargri muda umekimbia Claudio Marchissio sio yule wa miaka minne nyuma. Katika mchezo wa kwanza wa hatua ya kumi na sita bora watamkosa Paul Dybala ambae ni majeruhi.
             LIVERPOOL : wamefanya usajili mzuri katika dirisha la January kwa kumsalijili Virgil van Dijk kutoka Southampton kwa ada ya rekodi ya dunia kwa beki. Walitolewa mapema katika kikombe cha ligi (carabao cup) na hivi majuzi walitolewa katika kombe la FA wapo nyuma kwa  pointi nyingi sana dhidi ya vinara Manchester city wamempoteza Phillipe Countinho na hawajatafuta mbadala wake ijapo kuwa bado ni timu nzuri wanakwenda kwa FC Porto katika kiwango chake kisicho haba.
             CHELSEA : kilio kikuu cha kocha Antonio Conte pale Stanford bridge ilikua ni ufinyu wa kikosi na mlolongo wa ratiba. Hili la usajili mabosi wakilisikia na kumuongezea nguvu katika kikosi dirisha hili la January Ross Barkley Emerson na Olivier Giroud ni moja kati ya wachezaji wapya wa  Chelsea,hawajawa na mwenendo mzuri sana wa matokeo wakiwa wametolewa katika kombe la ligi (carabao cup) wakiwa nyuma kwa pointi nyingi dhidi ya vinara Manchester city. Kimbilio lao kwa sasa ni ligi ya mabingwa mbele ya Barca katika ubora wao.
             TOTTENHAM HOTSPURS : kwa misimu kadhaa wamekua wasindikizaji katika kombe hili wakitolewa katika hatua ya makundi, msimu huu wameonekana kuimarika na kukomaa zaidi hawapo katika mbio za ubingwa baada ya tofauti ya pointi 20 kati yao na vinara Manchester city. Wakitolewa katika kombe la ligi na watalazimika kurudiana tena katika kombe la FA ili kuweza kusonga mbele. Wanakikosi kizuri japo si wazuri katika mechi za ugenini wanapocheza na timu kubwa. Wamejaribu kulizipa pengo la Kyle Walker lakini Kelvin Trippier bado hajawa vizuri kuvaa viatu vyake.
        MANCHESTER UNITED : walianza msimu huu kwa kasi wakishinda goli nne mfululizo lakini mambo hayajawa mazuri kwao kwa kipindi hiki. Wapi nyuma kwa pointi 15 dhidi ya vinara Manchester city walitolewa na Bristol city katika kombe la ligi na wamesonga mbele katika kombe la FA. Wamemuongeza Alexis Sanchez katika kikosi chao na wanatarajia watafanya vizuri.
             Kuna rafikiangu mmoja amewahi kuniuliza kwanini mpira ni pointi tatu na si moja? Nilijaribu kutafakari na kujaribu kumjibu kuwa mpira ni matokeo matatu yaani ushindi suluhu au kufungwa lakini mshindi hubeba vyote na mkitoshana nguvu basi ya bidi kugawana alama. Tukutane kule Ukraine katika jiji la Kyiv kuangalia wanaume 22 wakitoana jasho na baada ya hapo tuwahi kule Russia kuweka vyumba tukisubiri kombe la dunia.

0 comments:

Post a Comment